RAILA ODINGA AJIONDOA KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO KENYA
Kiongozi
mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hatashiriki kwenye
uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
Bwana
Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama
ya juu.
Uchaguzi
huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu
nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Bw.
Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa kutosha
kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa njia nzuri.
Awali
tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa
mshindi.Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura milioni 1.4.
Upinzani
nchini Kenya awali ulikuwa umetangaza wazi kuwa ungeshiriki kwenye uchaguzi
mkuu ikiwa mabadiliko yanayostahili yangefanyika.
Upinzani
unaamini kuwa uchaguzi unastahili kufutwa baada ya Odinga kujiondoa, na kutoa
muda wa kutosha kufanyika mabadiliko yanayostahili ili uchaguzi kufanyika kuambatana
na sheria na katiba.
Serikali
imekuwa ikisema kuwa uchaguzi utafanyika na rais kuapishwa.Bw. Odinga pia
ametoa wito kwa watu kuandamana Jumatano hii kwa kutumia kauli mbiu
"hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi".
Mwezi
Septemba mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriako Tobiko, aliamrisha polisi
na tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza ikiwa wanachama wa tume ya uchaguzi
walihusika na uhalifu wowote.
Alitaka
wachunguzi kuchunguza madai kuwa maafisa wawili wakuu wa upinzani walikuwa
wamedukua mitandao ya tume ya uchaguzi.
Comments