CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI KATAVI CHAFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI WILAYANI TANGANYIKA
Na.Issack Gerald-Katavi
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoani
Katavi,kimefuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Bw.Yasin Mohamed
Kibiriti kuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Tanganyika.
Katibu wa chama hicho Mkoani Katavi
Bw.Kajoro Peter Vyohoroka pamoja na mambo mengine amesema kamati ya Halmashauri
kuuya CCM mkoani Katavi imeamua kufuta matokeo ya uchaguzi wa ccm wilayani
Tanganyika katika nafasi ya Mwenyekiti,Katibu wa
siasa na uenezi na wajumbe wote wa kamati ya siasa ya Halmashauri kuu.
Amesema
sababu ya kufuta matokeo hayo ni kutokana na mwenyekiti anayetakiwa kushindwa
kupata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa huku mwenyekiti aliyekuwa
akidaiwa kushinda akitangzwa kinyume na kanuni za chama hicho.
Wakati
huo huo Msimamizi mkuu Bw.Chrisant Mwanawima amepatiwa adhabu kwa mjibu wa
kanuni na maadili ya chama kwa kushindwa kwake kusimamia uchaguzi huo huku
akijua kuwa anavunja kanuni ya uchaguzi kwa kuwa wakati anatangaza matokeo
hakumshirikisha msaidizi wa uchaguzi ambapo ilionekana ilikuwa ni kumpendelea
Bw.Yasin Kibiriti.
Kwa mjibu
wa matokeo yaliyotangazwa Yasin Mohamed Kibiriti alipata kura 222,Abdallah
Salum Sumry kura 175,Mombo Rashid Mombo kura 53 ambapo jumla ya kura
zilizopigwa zilikuwa 458,kura halali 450 huku kura 8 zikiharibika.
Kikao
maalumu cha kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM
Mkoani Katavi chini ya mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Mselem
Abdallah Said kilikutana Juzi Oktoba 9,baada ya kupokea malalamiko juu ya
uchaguzi uliofanyika Oktoba 6 mwaka huu.
Kwa mjibu
wa Katibu wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Kajoro Peter Vyohoroka msimamizi wa
uchaguzi hakuzingatia kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2012 ibara ya 11(b) na Ibara
ya 21(b).
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments