RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MASENETA WA MAREKANI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
leo amekutana na Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wengine wa Baraza la
Marekani Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli ameupokea ugeni huo na kufanya nao mazungumzo
mbalimbali ndani ya Ikulu. Hata hivyo bado taarifa rasmi za nini haswa
wameongea viongozi hao baada ya kukutana hazijatoka.
Pia leo Rais Dkt. John Pombe Magufuli
amempokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan
alipotembelea Ikulu na kuteta mambo na mheshimiwa Rais.
Aidha Rais Dkt. Magufuli amepokea kitabu cha Seneta James Inhofe
kilichoonyesha picha za maeneo mbalimbali ya Tanzania alipotembelea mwaka mmoja
na nusu uliopita.
Comments