VIONGOZI WENGINE WALIOWAHI KUAPISHWA NA KUJITANGAZA KUWA MARAIS KAMA ODINGA BARANI AFRIKA
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumanne aliapishwa kuwa 'rais wa wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana. Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza kwa sherehe hiyo ya kuapishwa, ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa. Bw Odinga alisema Bw Musyoka, ataapishwa "baadaye". Waziri mkuu huyo wa zamani hayuko peke yake katika kujaribu kujitangaza marais, kukiwa bado kuna rais mwingine madarakani. Raila Odinga Akiapa Wengine ni akina nani? Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na orodha hii. Etienne Tshisekedi Etienne Tshisekedi Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinza...
Comments