RC KATAVI : WAZAZI MKOANI KATAVI WANAOKATISHA MASOMO WATOTO WAO KUKIONA CHA MOTO
Na.Issack
Gerald-Katavi
MKUU
wa mkoa wa Katavi Meja jenerali mstaafu Raphael Mugoya Muhuga,amesema serikali
itaendelea kuchukua hatua kali za kisheri dhidi ya wazazi wanawakatisha masomo
wanafunzi kwa tamaa ya kujipatia mahali.
Muhuga
ametoa kauli hiyo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani
ambayo kimkoa yameadhimishwa katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili Manispaa
ya Mpanda.
Aidha
Mkuu wa Mkoa amesema ripoti ya vifo vya uzazi vinavyotokea Mkoani Katavi inaonyesha
hutokana na mimba katika
umri mdogo kwa wasichana wenye umri
kati ya miaka 15 hadi 18.
Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Mpanda Agness
Buraganya pamoja na mambo mengine amewataka wazazi na walezi kuachana na tamaduni za kizamani kwa kuona kuwa mtoto wa
mwenzie haifai kumkanya anapokosea masuala kadhaa.
Wakati
wa kongamano la siku hiyo lililofanyika jana Mjini Mpanda likishirikisha wadau
mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,ripoti katika mkoa wa Katavi inaonesha
katika kipindi cha 2012-2016 wanafunzi wapatao 258 walikatizwa Masomo kwa
sababu ya mimba.
Hata
hivyo huenda takwimu hizo zikawa zimeongezeka mpaka kufikia mwaka huu kwa kuwa
katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu,mimba kadhaa za wanafunzi
zimeripotiwa katika Halmashauri za Mkoa wa Katavi ikiwemo Halmshauri ya Wilaya
ya Nsimbo yenye wanafunzi 14 waliopatwa na mimba katika kipindi cha miezi sita
iliyopita.
Siku
ya mtoto wa kike duniani iliasisiwa na umoja wa mataifa Desemba 2011 lengo likiwa kutafuta shida na
dhuluma kwa mtoto wa kike katika mataifa mbalimbali.
Katika
maadhimisho hayo ambayo kitaifa yameadhimishwa Wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo
“Kauli mbiu inasema tokomeza mimba za
utotoni kufikia uchumi wa viwanda”
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blohspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments