WASIOJULIKANA WAMEUA MTU KWA RISASI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-Tanganyika Katavi
ACP Damas Nyanda |
Akithinitisha tukio hilo Kamanda wa
Polisi Damasi Nyanda amesema tukio hilo limetokea jana usiku wa saa mbili
wakati wanafamilia hao wakiangalia taarifa ya habari ambapo inadaiwa watu hao
waliomba maji ya kunywa na baadaye kufanya uhalifu
huo.
Mwanamke huyo ni mke wa mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Katavi (CCWT).
Mwanamke huyo ni mke wa mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Katavi (CCWT).
Tukio
lingine limetokea majira a sasa saba usiku katika kijiji cha Kabage B kilichopo
wilayani Tanganyika Mama mmoja ameuwawa kwa kukatwa na Mapanga na watu wasio
julikana.
Kamanda
Nyanda amewaasa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapo baini
uwepo wa vitendo vya uharifu ili sheria ichukue mkondo wake.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando amewataka wananchi
wanao miliki silaha kinyume na utaratibu wazisalimishe katika jeshi la polisi
kabla ya hatua kuchukuliwa.
Kumeendelea kujitokeza wimbi la uhalifu wa matumizi ya silaha za moto pamoja na matukio ya ukataji wa mapanga huku mengine yakihusishwa na imani za kishirikina Wilayani humo.
Kumeendelea kujitokeza wimbi la uhalifu wa matumizi ya silaha za moto pamoja na matukio ya ukataji wa mapanga huku mengine yakihusishwa na imani za kishirikina Wilayani humo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments