MBUNGE MPANDA VIJIJINI:WILAYA YA TANGANYIKA IMETENGEWA VISIMA 21 MWAKA 2017/2018
Na.Issack
Gerald-Tanganyika Katavi
WILAYA ya Tanganyika imetengewa
visima 21 vya maji safi na salama katika mwaka wa fedha 2017 na 2018.
Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la
Mpanda vijijini Suleimani Kakoso katika kikao cha kwanza cha Baraza la madiwani
halmashauri ya wilaya ya Mpanda kinacho fanyika katika ukumbi wa Idala ya maji.
Ameongeza kusemakuwa bado
kunajitihada nyingi zinazofanywa na serikali kwa
kushirikiana na wadau mbali mbali kuhakikisha wananchi wa wilaya hiyo Changa
wanaondokana na adha ya maji.
Mapema
mwaka 2017 katika kata ya Majalila iliyopo wilayani Tanganyika ulizindua mradi
mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya milioni 600 yanayo sukumwa kwa nishati
ya jua.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments