TANROADs MKOANI RUKWA WASHAURIWA KUPUNGUZA MATUTA
MKUU
wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa ameishauri wakara wa barabara nchini
Tanroads mkoani Rukwa kupunguza idadi ya matuta yaliyopo barabarani kati ya
Sumbawanga mjini na kijiji cha mkutano ambacho ndio mpaka wa mkoa wa Rukwa na
Songwe kwani imekuwa nichanzo cha ajali.
Akizungumza
katika kikao cha kamati ya ushauri ya barabara mkoa wa Rukwa alisema kuwa
katika barabara hiyo ya Sumbawanga Mbeya matuta yamezidi kiasi kwamba yamekuwa
nikero.
Alisema
kuwa katika kipande hicho cha barabara chenye urefu wa kilomita 150 kinamatuta
139 ambayo ni mengi na nihatari kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kwani
yamezidi kiwango.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikitokea kwani matuta hayo
yamekuwa yakichangia magari kupoteza muelekeo nivizuri ya kapunguzwa kwa
usalama wa watumiaji wa barabara.
Wakati
wa kikao hicho,mwenyekiti wa wakandarasi mkoa wa Rukwa Anyosisye Kiluswa
alisema kuwa imefika wakati wakandarasi wazalendo wa anzekupewa kazi za daraja
la 7 mpaka la tano kwani kazi hizo wamekuwa wakishindania na makampuni makubwa
na yamekuwa yakishinda hivyo wakandarasi wazawa kukosa kazi na kushindwa
kuchangia pato kwa kulipa kodi.
Alisema
Tanroads itoe upendeleo maalumu kwao na makampuni makubwa yapewe kazi za daraja
la 4,3,2 na kuendelea ambazo zinahitaji mitaji mikubwa na teknolojia kubwa
ambayo wakandarasi wazawa hawana uwezo nazo.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa inapotokea barabara za mkoa huo zinapo haribika wanapewa
wakandarasi wadogo kuzifanyia ukarabati hivyo kujikuta hawana mitaji yakufanya
kazi hizo kutokana na kutopata kazi.
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la Kwela Ignas Malocha alichangia katika kikao hicho
alisema kuwa bado barabara za mkoa huo zinakabiliwa na changamoto ya wafugaji
kupitisha mifugo yao barabarani kwa kuiswaga badala ya kuipakiza katika
malori.
Alisema
kitendo hicho kinasababisha uharibifu mkubwa wa barabara na kikiendelea
kufumbiwa macho kitaendele kuharibu miundombinu hiyo.
Kwaupande
wake mkuu wa mkoa huo ambaye pia ndiyo mwenyekiti wakikao hichoaliwaagiza
Tanroads pamoja na TARURA mkoani humo kuhakikisha barabara zinakuwa bora wakati
wote na kupitika bila usumbufu ikiwa ni pamoja na kuanza kufikilia barabara
mbadala ili kuanza kujipanga kukabiliana nafoleni za magari siku zijazo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments