BANGI,NYARA ZA SERIKALI ZAWAPELEKA WATU 40 MIKONONI MWA POLISI
JESHI la polisi mkoani Dodoma
linawashikilia watuhumiwa 46 wa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na nyara za
serikali zenye dhamani ya zaidi ya shilingi million 20.
Watuhumiwa hao wamekamatwa katika
oparesheni iliyofanywa kuanzia octoba 4 hadi 12 mwaka huu ikihusisha taasisi
mbalimbali zikiwemo shirika la umeme nchini (TANESCO), Mamlaka ya chakula na
dawa nchini (TFDA),Uhamiaji,Maliasili na Polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi
mkoani Dodoma Gilles Muroto,amesema katika oparesheni hiyo zimekamatwa nyara za
serikali ambazo ni ngozi mbili za mnyama aina ya chui zenye thamani ya shilingi
milioni 15,750,000,nyama ya mnyamapori aina ya tandara kilogram tatu zenye
thamani ya sh. 5,700,000.
Katika
hatua nyingine Jeshi hilo limekamata pikipiki tano za wizi pamoja na pikipiki
zaidi ya 500 zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.
Wakati huo huo amesema kuhusu mazao ya misitu walikamata mbao 200,mkaa pamoja na makosa ya kuharibu misitu na kufanya shughuli za kuchoma mkaa katika maeneo ya hifadhi.
Wakati huo huo amesema kuhusu mazao ya misitu walikamata mbao 200,mkaa pamoja na makosa ya kuharibu misitu na kufanya shughuli za kuchoma mkaa katika maeneo ya hifadhi.
Hata
ameonya tabia ya baadhi ya wazazi kuingia mkataba na dereva wa bodaboda kupakia
watoto kuwapeleka shuleni na kuwarudisha nyumbani ambapo kamanda Muroto
amewataka waalimu kutowapokea wanafunzi wanaotumia usafiri huo.
Oparesheni
hiyo pia ilishirikisha mataifa wanachama wa shirikisho la polisi Afrika
mashariki na kusini mwa afrika chini ya shirikisho la polisi Interpol ,lengo
likiwa ni kukabili hali ya uharifu wa makosa mtambuka yanayovuka mipaka ya
nchi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments