BENK YA TANZANIA BOT YATOA SEMINA KWA WATU WENYE ULEMAVU NAMNA YA KUTAMBUA FEDHA HALALI
WATU wenye ulemavu wakusikia(viziwi)mkoani Rukwa wameishukuru Benki kuu ya Tanzania kwa kuwapa mafunzo maalumu ambayo yamewajengea uwezo wa kutambua namna bora ya kuhifadhi fedha sambamba na kujua tofauti ya fedha halali na bandia.
Mafunzo
hayo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa Moraviani
Conference yalihusisha watu wenye ulemavu wakutosikia ambapo walifundishwa
namna bora yakuhifadhi fedha pindi waendapo katika matumizi kwani watu wengi
wamekuwa hawajui namna bora ya kuweka fedha zao.
Akizungumza
katika Mafunzo hayo meneja msaidizi idara ya Benki kuu Tanzania Vick
Msina,alisema kuwa watu wengi wamekuwa hawajui namna bora bora ya kuweka hela
kwani wamekuwa wakizikunja nakuziweka mifukoni ama wanawake kuzifunga katika
kanga walizo vaa kitendo kinacho sababisha hela hizo kuchakaa mapema.
Alisema
ni vizuri mtu yeyote anapokuwa anakwenda kufanya manunuzi akawa anabeba hela
kwenye pochi zikiwa zimenyooka badala ya kuzikunja na kuweka mfukoni,ana kuweka
miguuni kwenye soksi ama kwenye sidiria kwani kufanya hivyo kunasababisha hela
kuchakaa haraka.
Huyo
alisema kuwa suala hilo si tu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia bali ni jukumu
la kila mwananchi kuhakikisha kuwa ana zitunza fedha vizuri ili zitumike kwa
muda mrefu.
Naye
mwenyekiti wa viziwi mkoa wa Rukwa Henry Kisusi alisema kuwa mafunzo hayo
yamekuwa nimuhimu sana kwao kwani wamekuwa hawapati fursa nyingi na hivyo
kujikuta wakitumia vibaya fedha hizo pamoja na kubambikiziwa fedha bandia.
Awali
akizungumza katika mafunzo hayo mwenyekiti wa kituo cha viziwi nchini Habib
Mlope alisema kuwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwemo viziwi
wanatakiwa kupewa mafunzo mara kwa mara yatakayo wasaidia katika kukabiliana na
changamoto mbalimbali hususani katika zama hizi ambazo baadhi ya watu wanapenda
kuendesha maisha kwanjia ya utapeli.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments