ULINZI SHIRIKISHI UMESAIDIA KUTOKOMEZA UHARIFU MKOANI TABORA
Emeelezwa kuwa kuwepo kwa vikundi vya
ulinzi shirikishi katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tabora kumesaidia
kupunguza vitendo vya uharifu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watu wasio
waadilifu mkoani humo.
Hayo yamesemwa leo na kamanda wa
jeshi la polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi ACP
Wilbroad Mutafungwa.
Kamnada Mutafungwa amesema jeshi la polisi mkoani humo limekuwa likitoa askari mmoja kwa kila mtaa ambao unakikundi cha ulinzi shirikishi ili kuimarisha doria katika mitaa hiyo.
Kamnada Mutafungwa amesema jeshi la polisi mkoani humo limekuwa likitoa askari mmoja kwa kila mtaa ambao unakikundi cha ulinzi shirikishi ili kuimarisha doria katika mitaa hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa jeshi la Sungu sungu katika kijiji cha Mwanihalanga
kata ya Mbutu wilayani Igunga amesema katika kijiji chao hupanga watu kumi kwa
ajili kushiriki kwenye ulinzi shirikishi wakati wa usiku na asiyetaka hutozwa
faini.
Nao
Baadhi ya wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa mbalimbali mkoani humo
wamesema wao hushirikiana vizuri na askari wa jeshi la polisi katika kuimalisha
doria katika mitaa yao na kuwaripoti watu wageni wasiowatambua ambao hufika
katika maeneo yao.
Mmoja wa
wakazi waliowahi kuibiwa Bi Asha Jacobo kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi
shirikishi katika mtaa wake amesema ulinzi shirikishi katika jamii ni muhimu
kwa kuwa bila ulinzi ndiyo maana hata yeye alibiwa mali yake.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments