MKUU WA MKOA WA RUKWA AIONYA TARURA
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameutahadharisha Wakala wa
Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na
Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.
Amesema
kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa
chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya
mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia
ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.
“Ukiitwa
Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi
ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo
mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini
kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona
mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote
alifafanua.
Ameyasema
hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa
fedha 2017/2018.
Amesisitiza
kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za
kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano
inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.
Hivyo
ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na
kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na
hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments