KUU WA MKOA WA RUKWA ATAKA VIKAO VYA DCC VIFANYIKE
MKUU
wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven ameagiza kuanza kufanyika vikao vya kamati ya
maendeleo ya wilaya (DCC) kwani vimekuwa havifanyiki kwa muda mrefu.
Akifungua
jana kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Rukwa(RCC) alisema kuwa kwa muda
mrefu sasa vikao hivyo havijafanyika kwa kisingizio cha kutokuwa na posho kitu
ambacho siyo sahihi.
Alisema
kwa ngazi ya mkoa kikao hicho kimekuwa kikifanyika bila posho Lakini cha
kushangaza kwa ngazi ya wilaya vikao hivyo havifanyiki.
Aliwasihi
watumishi wa umma Kuongeza kasi katika kuwatumikia wananchi kwani dunia hivi
sasa imebadirika lazima tukimbie wakati wengine wanakimbia mkoa wa Rukwa
unahitaji maendeleo kwa kasi kubwa.
Katika
kikao hicho mmoja wa wajumbe waalikwa Zeno Nkoswe alipendekeza kuwa imefika
wakati sheria iliyoanzishwa kuanzisha kikao hicho cha itazamwe upya uwakilishi
uongezwe kwani wajumbe halali ni 28 ambao wanawakilisha wakazi zaidi ya milioni
1 wamkoa huo.
Nkoswe
alisema kuwa kutokana na zama tulizonazo nivema idadi ya wajumbe wakikao hicho
ikaongezeka kwa uwakilishi, tofauti na sasa walio wengi ni waalikwa ipo siku
wanaweza wasije kwakua hawabanwi na sheria.
Pia
alisema kuwa wakulima wamekata tamaa kutokana na kutokuwa na soko la zao la
mahindi kwani wakulima wa mahindi hawana kwa kuyauza,wanakabiliwa na hali ngumu
kiasi kwamba mkulima anaona kama kazi hiyo ni laana kutokana na ugumu wa maisha
na hata wakiyauza humu nchini wanayauza kwa shilingi 40,000 kwa gunia bei
ambayo haiwalipi.
Kwaupande
wake Askofu wa kanisa la Moravian Dayosisi ya Sumbawanga Conrad Nguvumali
alisema kuwa hivi sasa wakulima wamegeuka kuwa wafanyabiashara ya magendo kwaku
waserikali imezuia kuuza mahindi nje ya nchi badala yake wakulima wanayatorosha
mahindi nyakati za usiku kwakutumia punda na baiskeli.
Naye
Mbunge wa Nkasi kusini Desderius Mipata alise makuwa mvua zimeanza kunyesha na
mawakala bado hawajalipwa madeni yao huwenda wakashindwa kusambaza pembejeo kwa
wakulima.
Alisema
kuwa hali ya mawakala ni mbaya sana wengi wamefilisika na nyumba zao zinapigwa
mnada na mabenki kutokana na mikopo waliyochukua kufanya kazi hiyo hivyo
serikali iwalipe ili kuwakomboa.
Naye
Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Kessy alisema kuwa vituo vya hali ya hewa vina
majengo mazuri lakini sio msaada kwa wakulima kwani havitoi taarifa ya
hali yahewa ipasavyo kwa wakulima.
Mwisho
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments