WANANCHI WILAYANI TANGANYIKA WAMETAKIWA KUWASILISHA MALALAMIKO YA MIGOGORO YA ARDHI BADALA YA KUJENGA KIHOLELA
Na.Issack
Gerald-Tanganyika
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi imetoa wito kwa wakazi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha malalamiko yao
kuhusu migogoro ya ardhi badala ya kuamua kujenga kiholela katika maeneo
yasiyoruhusiwa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa idara
ya ardhi na maliasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bi.Josephine Beda
Lupia wakati akizungumzia kuhusu mikakati iliyowekwa kudhibiti wakazi
wanaojenga makazi holela katika maeneo yasiyo rasmi.
Aidha Bi.Lupia amesema katika kuweka
matumizi bora ya ardhi,halmashuari kwa kushirikiana na baraza la madiwani
katika halmshauri hiyo,walipitsha kutengwa zaidi ya hekta 46,000 kwa ajili ya sekta ya
kilimo,uwekezaji na ufugaji.
Katika hatua nyingine Bi.Lupia
amesema katika mpango bora wa ardhi,walizingatia pia haki za makundi maalumu
yasiyokuwa na uwezo kwa kulipia fedha taslimu na badala yake wakapewa nafasi ya
kulipa kwa awamu ambapo jumla malipo yalikuwa hadi shilingi laki moja kwa
kiwanja.
Maeneo yaliyokuwa yakitajwa kuvamiwa
na wakazi kuendesha shughuli mbalimbali bila kuidhinishwa kuwa makazi rasmi ni
pamoja Misanga,Lyamgoroka na Mnyamasi.
Habari zaini ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania.blogspot.com
Comments