CWT MKOANI KATAVI KIMEZUNGUMZIA SHULE ZA SERIKALI KUFANYA VIBAYA MTIHANI WA DARASA LA SABA MWAKA 2017.
Na.Issack Gerald-Katavi
CHAMA cha walimu Tanzania CWT mkoani
Katavi kimesema wanafunzi wengi wa shule za serikali wanashindwa kufaulu vizuri
kwa kiwango cha juu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlundikano wa
wanafunzi wengi darasani kwa wakati mmoja.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa
CWT Mkoani Katavi Hamisi Ismail ambapo amesema shule za binafsi zinafanya
vizuri katika kufaulisha wanafunzi kutokana na kuwa na idadai ndogo ya
wanafunzi darasani idadi ambayo ni rahisi mwalimu kuimudu anapokuwa anafundisha
suala ambalo limekuwa gumu upande wa shule za serikali.
Katika hatua nyingine amesema uwepo
wa vitabu vingi vyenye mitaala inayotofautiana husababisha wanafunzi kuelewa
mambo tofauti akisema kuwa ni vema serikali ikawa na kitabu kimoja
kitakachotumika nchi nzima.
Wakati huo huo Mwalimu Hamisi Ismail
amesema chama cha walimu CWT mbali na kuwepo kwa ajili ya kutetea haki na
maslahi ya walimu,pia kinahakikisha walimu wanawajibika katika kufundisha
wanafunzi ipasavyo pamoja na kuzingatia maadili mema.
Kauli ya chama inakuja ikiwa ni siku
chache baada ya Baraza la Mitihani Tanzania NACTE kutangaza matokeo ya mtihani
wa darasa la saba ambapo imeonekana shule za serikali zimefanya vibaya kuliko
shule zinazomilikiwa na watu binafsi.
Comments