MWAFAKA WA UGAWAJI VIWANJA KUPATIKANA LEO MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-Katavi
SERIKALI za mitaa ya Msasani na
Tambukareli Manispaa ya Mpanda,leo zinatarajia kufanya mkutano wa hadhara kwa
ajili ya kupata mwafaka wa namna ya kugawa viwanja kwa wahanga wa bomoa bomoa.
Mwenyekiti wa mtaa wa Msasani
Bw.Jonard Makoli amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia majira ya
saa 8 mchana.
Mkutano huo unafanyika ikiwa tayari
kuna malalamiko kutoka kwa wakazi wa mitaa ya Msasani na Tambukareli
wakilalamika kutoridhishwa na mfumo wa ugawaji viwanja ambapo imeelezwa kuwa
watakaopewa kipaumbele ni watu wasiokuwa na uwezo kama wazee na wagonjwa huku
wananchi wengine wakisema ni mpango unaowaacha bila kujua hatima yao.
Viwanja 150 vilivyopo mtaa wa Kampuni
kata ya Misunkumilo vilinunuliwa na
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mh.Sebastian Kapufi ili vigawiwe bure kwa
wakazi hao ambapo kwa mjibu wa Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Willium
Mbogo kila mtaa utapata viwanja 75 kwa ajili ya wakazi wake.
Zaidi ya Kaya zipatazo 200
zinatarajiwa kubomolewa makazi yao ili kupisha bomoabomoa ili eneo la hifadhi
ya reli ibaki wazi na wakazi hao wanatakiwa wawe wameondoka kabla ya mwezi
Januari mwakani.
Comments