WAKULIMA WA KAHAWA KUTOKA KIGOMA KWENDA IKULU YA RAIS KUFIKISHA KILIO CHA MADAI YAO
Chama cha ushirika cha wakulima wa kahawa (AMKOS)
wilayani Buhigwe mkoani Kigoma,kimechagua wawakilishi watatu,kwa ajili ya kuwawakilisha
wakulima hao kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.
Wawakilishi hao watamfikishia Mh.Rais madai yao wanayodai kwa
viongozi waliopita wa chama hicho,ambapo ni muda wa miaka miwili sasa.
Wamefikia maamzi hayo katika mkutano wa wanachama uliofanyika
wilayani humo,kwa lengo la kujadili kuhusu madai yao wanayodai kwa viongozi
waliopita wa chama hicho.
Mwenyekiti wa chama hicho,Bw.Issa Madamu amesema, wakulima
hao wanadai jumla ya sh.mil.27 kwa viongozi hao waliopita tangu 2015.
Bw.Madamu amesema juhudi za kudai pesa hiyo,zimeenda hadi
ngazi ya mkoa lakini bado hawajapata mafanikio na kwamba ndio maana wamechukua
maamzi hayo ya kwenda kwa Rais ili wapatiwe ufumbuzi wa madai yao.
Aidha wakulima hao wameiomba serikali ya mkoa wa Kigoma kuwahimiza
viongozi wa ngazi za chini kushughulikia matatizo ya wananchi wa hali ya chini
ili kukuza na kuleta maendeleo kama Mh.Rais Magufuli anavyoagiza.
Comments