KAULI YA KAMANDA WA POLISI TABORA HII ITAZAA MATUNDA?AU NI DANGANYA TOTO?
Kamanda
wa Jeshi la polisi mkoani Tabora ACP Wilbrod Mutafungwa amewataka wananchi waliokimbia
hivi karibuni kwenye kijiji cha Mwamabondo kurejea katika makazi yao.
Wakazi
hao walikimbia kufuati msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi
baada ya wananchi hao kufanya jaribio la kutaka kuwaua wanawake
wanne waliowapiga na kuchomwa moto sehemu za siri kutokana na imani za
kishirikina.
Aidha
Kamanda Wa Polisi Mkoani Tabora Amelazimika Kusafiri Umbali Mrefu Wa Zaidi Ya
Kilometa 150 Kwa Ajili ya Kuzungumza na baadhi ya wananchi waliobakia
Kijijini Hapo.
Wakati
akizungumza na wananchi hao miongoni mwa mambo yaliyojitokeza Katika Mkutano huo
ni pamoja na kuelezwa kuwa Mahudhurio ya wanafunzi wa shule ya msingi kijijni
hapo yameshuka kwa asilimia 30 kutokana na wazazi wa wanafunzi hao kukimbia kutakimbia
makazi yao.
Miongoni
mwa Wanawake wanne walionusurika kifo wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuokoa
maisha yao.
Mwanzoni
mwa mwezi wa tisa mwaka huu wananwake 4 wakazi wa kijiji cha Mwamabono wilayani
Uyui walinusurika kufa baada ya kupigwa na kuchomwa moto sehemu zao za siri
kutokana na imani za kishirikina wakidaiwa kuhusika na kifo cha mganga mmoja
kijijini hapo.
Hiki
ni Kijiji Cha Mwamabondo Kilichopo Kata Ya Loya Wilayani Uyui Mkoani Tabora,wakazi
wake Wanajishughulisha Zaidi na shghuli za kilimo.
Comments