WANANCHI MKOANI TABORA WAMETAKA KITUO CHA POLISI KIFUNGULIWE
Wananchi
wa kata ya Loya wilaya ya uyui mkoani tabora wameomba kufunguliwa kituo cha
polisi katani humo kwa lengo la kukabiliana na matukio ya uharifu.
Kata
hiyo pamoja na kata nyingine nne hazina kituo cha polisi hali inayowalaizimu
kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 150 kufuata huduma za kipolisi katika kata
ya Kigwa.
Wakizungumza
katika mkutano wa hadhara mbele ya kamanda wa polisi mkoa wa tabora ACP Wilbrod
Mutafungwa wananchi hao wamesem kwa sasa wanakabiliwa na matukio mbalimbali ya
uharifu ikiwemo wizi lakini imekuwa vigumu kudhibiti uharifu katika maeneo hayo
kwa kuwa hakuna kituo cha polisi.
Kamanda
Mutafungwa baada ya kukagua jengo la kituo cha polisi katani hapo,ametoa muda
wa wiki mbili kwa viongozi wa kata na wilaya kukamilisha ukarabati wa jengo la
kituo cha polisi ili kifunguliwe na kuanza kuwahudumia wananchi.
Wananchi
wa kata ya Loya na kata jirani wanaamini kufunguliwa kwa Kituo hicho cha polisi
kitakuwa mkombozi wa matukio mbalimbali ya uharifu.
Comments