WANAFUNZI 5 NA MLINZI WAMEKUFA KWA WAPIGWA RISASI
Mashahidi wanasema watu watatu waliokuwa na silaha,mmoja wao
akiwa mwanafunzi wa zamani walivamia mabweni katika Shule ya Upili ya
Lokichogio leo asubuhi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo anasema mshambulizi mkuu alikuwa
mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo aliyefukuzwa kwenda shuleni baada
kupigana na mwenzake ambapo alikuwa ameagizwa kurudi na wazazi wake lakini
hakufanya hivyo.
Walioshuhudia walisema mwanafunzi huyo alirudi shuleni usiku
wa manane na wenzake wawili ambapo inadaiwa walimpiga risasi na kumuua mlinzi
na kisha kwenda katika mabweni wakimtafuta mwanafunzi waliyepigana naye awali.
Mwanafunzi huyo hakuwa shuleni wakati huo na washambuliaji
hao waliwapiga risasi na kuwaua wanafunzi watano na kuwabaka wasichana wawili.
Chama cha msalaba mwekundu kimesema kimewahamisha
waliojeruhiwa hadi hospitalini.
Lokochogio iko karibu na mpaka wa Sudan Kusini na Ethiopia na
wakaazi wengi wa eneo hilo hubeba bunduki na ni wachungaji wanaolinda mifugo wao
dhidi ya wizi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments