RAIS MAGUFULI-MWENYE UTAENDELEA NA MBIO ZAKE KAMA KAWAIDA NIKIWA MADARAKANI
Na.Issack Gerald-Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe
Magufuli amesema katika kipindi chake cha uongozi,Mwenge wa Uhuru utaendelea
kukimbizwa nchi nzima kila mwaka.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo mashinikzo
kutoka kwa watu mbalimbali nchini wakitaka mwenge wa uhuru ufutwe kwa madai
kuwa umekuwa ukiigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi chote
cha miezi 6 ambacho huwa unakimbizwa nchi nzima.
Rais Magufuli amesema miongoni mwa sababu zinazosababisha
mwenge huo usifutwe katika kipindi chake
ni kuwa,mwenge huo unachochea maendeleo ya nchi.
Kwa mjibu wa rais Magufuli,katika mbio za mwenge wa uhuru kwa
mwaka 2017,viwanda 148 vyenye thamani ya shilini mia nne na sitini na nane
vitakavyotoa ajira zaidi ya elfu kumi na na tatu vimezinduliwa nchi nzima.
Pia alisema anawashangaa wanaotaka mwenge huo ufutwe, kwani
wao ndio huwa mstari wa mbele kupokea Kifimbo cha Malkia au kushiriki kwenye
mwenge wa Olimpiki.
Sherehe za kuzima
mwenge wa uhuru zimesherehekewa sambamba na kilele cha wiki ya vijana pamoja na
kumbukumbu ya miaka 18 tangu kifo cha baba wa taifa hayati Julius nyerere
kilichotkea Oktoba 14 mwaka 1999.
‘’Kaulimbiyu kwa mwaka huu inasema shiriki kukuza uchumi wa
viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu’’
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments