SIMULIZI YA MAUAJI YA WANANDOA YALIYOTKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MKOANI KATAVI
Na.Issack
Gerald-Tanganyika Katavi
WANANDOA
Adamu Mtambo(41) na mkewe Catalina Mtambo(39
)wakazi wa Kitongoji cha Kasekese B Kata
ya Kasekese wilayani Tanganyika Mkoani Katavi
wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa wamelala
chumbani kwao.
Afisa Mtendaji
wa Kata ya Kasekese Ramadhani Ibrahimu alisema kuwa tukio hilo
lilitokea Jana majira ya saa 6:45 usiku nyumbani kwao.
Akielezea
tukio hilo alisema kuwa marehemu Adamu ambae alikuwa
ni mfanya biashara anamiliki
maduka mawili Kijijini hapo siku hiyo
alifanya biashara ya kuuza duka kama ilivyo kawaida yake
na baada ya muda wa kufunga duka ulipofika
alifunga na aliingia ndani kulala yeye na mke wake.
Wakati
wakiwa wamelala walikwenda wauaji hao ambao wanasadikiwa kuwa
walikua watatu na walifyatua risasi tatu za bunduki hewani ilikuwatisha
majirani ambao wangefika kutoa miaada, kisha
kuvunja mlango na kuingia ndani ya
chumba moja kwa moja walichokuwa wamelala wanandoa hao.
Afisa
mtendaji huyo alisema baada ya kuingia chumbani waliwakuta
wanandoa hao kitandani ndipo walipoanza kuwashambulia kwa kuwakata kata kwa
panga katika sehemu za usoni na kichwani
na kuwashambulia kwa kutumia malungu.
Wakiwa
wanawapiga marungu mwanaume alijaribu kuwasihi waache na na kuwaeleza
kama shida yao ni fedha yupo tayari kuwaonyesha mahali
zilipo lakini hawakuacha ndipo walipoanza kupiga makelele ya kuomba
msaada kwa majirani.
Alisema kutokana
na kelele hizo ndipo watoto wa marehemu ambao nao walikuwa
wakiishi kwenye nyumba hiyo wakiongozwa
na kaka yao aitwaye Charles
waliingia chumbani kwa wazazi wao kwa lengo la kutoa
msaada hata hivyo walishindwa baada
ya kushambuliwa na watu hao kwa kupigwa marangu hali iliyowalazimu
wakimbilie kwenye vyumba vyao vya kulala na kujifungua.
Hata
hivyo Majirani walifika kwenye eneo hilo na
kukuta mlango wa mbele ya nyumba ukiwa
umevunjwa na walipoingia kwenye chumba walichokuwa wanalala marehemu
hao waliwakuta wakiwa wamelala chini ya kitanda huku wakiwa na
majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za miili yao huku damu zikiwa
zimetapakaa chumbani na wauaji kutorokea kusikojulikana.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Kasekese Happnes Bona alisema
jitihada za kutafuta usafiri kwa ajiri ya kuwafirisha
wanandoa hao kuwapeleka hospitali ya wilaya ya Mpanda zilifanyika na
wakiwa njia walifariki.
Alisema
toka amekuwa mwenyekiti wa Kitongoji hicho hajawahi kuona
mauaji ya kutisha na yakikatili kiasi hicho kwani marehemu hao
waliuawa kwa kukatwa katwa kama wanyama.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda alipotafutwa majira ya saa
10 jioni ili kuelezea hatua ambazo zimechukuliwa na jeshi la polisi kutokana na
tukio hilo,kamanda Nyanda alisema hana taarifa kuhusu mauaji hayo.
Comments