OPAREHENI YANUKIA WILAYANI TANGANYIKA, USALAMA KWA RAIA UTAKUWEPO?
DC Tanganyika Salehe Mbwana Muhando |
Mkuu wa wilaya ya
Tanganyika Salehe Muhando amewataka wananchi wanaoishi Kalumbi katika kijiji cha Mpembe, Lyamgoloka
katika eneo la ushoroba wa wanyama,Igalukilo, Bariadi na Misanga Wilayani humo kuondoka haraka katika maeneo hayo.
Ametoa Tamko hilo leo
wakati na kusema kuwa tayari muda
uliokuwa umetolewa umekwisha.
Muhando amesema
wananchi wa Bariadi,Igalukilo na Misanga
wanatakiwa kurudi katika maeneo ya Luhafwe yaliyotengwa kwa ajili ya makazi yao
huku Wananchi wa kalumbi wakitakiwa kurudi katika eneo la makazi la kijiji cha
Mpembe.
Amesema kumekuwa na
matukio ya uvamizi wilayani humo mengine yakihusishwa na silaha za moto jambo
ambalo hutokana na watu kukaa katika maeneo yasiokuwa na Mamlaka kamili za
utawala na hivyo wahalifu kugeuza maeneo
hayo kama sehemu ya kujificha.
Hata hivyo kumekuwa na
malalamiko ya baadhi ya wakazi Wilayani Tanganyika kulalamika silaha za moto
kutumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya raia katika zoezi la
kuwaondoa wanaodiwa kuvamia maeneo ya hifadhi ambapo Oktoba 12 mwaka huu mtu
mmoja aliuawa na vyombo hivyo kwa kupigwa risasi na wengine saba kujeruhiwa.
Wakati huo huo wiki
iliyopita Mhando alisema wataendelea kutumia nguvu kuwaondoa wananchi wasiotaka
kuondoka kwa hiari katika maeneo ya hifadhi za misitu.
Wakati huo huo kumekuwa
kukiripotiwa matukio ya watu kuuwawa na watu wasiojulikana mkoani Katavi ambapo
karibu vifo vine vimeripotiwa.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments