MAUAJI TENA MKOANI KATAVI,SASA MITHILI YA KIBITI USIKU WA KUAMKIA LEO WASIOJULIKANA WAMEUA TENA MKE NA MME,KATIKA SIKU SABA IDADI YAFIKIA WATU 5 WAKIWEMO WANAOPIGWA KWA RISASI
Na.Issack
Gerald-Tanganyika Katavi
Watu wawili mke na Mme wanaofahamika kwa majina ya Adam
Charles (41) na Katalina Gabriel (39) wakazi wa Kijiji cha Kasekese Wilaya ya Tanganyika
Mkoani Katavi kwa kukatwakatwa na vitu vinavyosemekana kuwa vyenye ncha kali na
watu wasiojulikana.
Inaelezwa kuwa walivamiwa usiku wa saa 7 kuamkia leo na
kukatwakatwa sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za kichwani.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasekese Ramadhani Ibrahimu amethibitisha
kutokea kwa mauwaji hayo na jinsi tukio lilivyotokea.
Ibrahim amesema baad aya tukio hilo
walitoa msaada wa haraka kuwafikisha hospitali Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa
ajili ya Matibabu ambapo licha ya jitihada zao zote ili kuokoa maisha ya wawili
hao imehindikana na hatimaye kupoteza maisha.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia
tukio hilo na kutoa Msaada wameeleza kusikitishwa na tukio hilo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
Katavi ACP Damasi Nyanda alipotafutwa majira ya saa 10 jioni ili kuelezea hatua
ambazo zimechukuliwa na jeshi la polisi kutokana na tukio hilo,kamanda Nyanda
alisema hana taarifa kuhusu mauaji hayo.
Kuanzia Oktoba 7 mwaka huu,mpaka sasa
matukio yapatayo matatu yametokea na kupelekea mauaji kwa watu 5 wilayani
Tanganyika.
Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja
na tukio lililotokea Oktoba 7 likihusisha mtu mmoja mkazi wa kitongoji cha
myamasi aliyeuawa kwa kupigwa risasi ambapo kwa mjibu wa mwenyekiti wa
kitongoji cha Mnyamasi mkazi huyo,alipigwa risasi na vyombo vya kamati ya ulizi
na usalama vilivyokuwa vikifanya zoezi la kuwaondoa wavamizi wa hifadhi ya
misitu Wilayani Tanganyika.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe
Mhando alithibitisha mtu huyo kuuwawa akisema kuwa amepigwa risasi katika
majibizano kati ya raia na vyombo vya kamati ya ulinzi na usalama ambapo pia
inaelezwa watu 7 walijerehiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
MATUKIO YA HIVI KARIBUNI
Ripoti za Oktoba 12,2017
Mtu mmoja anayefahamika kwa jila la Suzani Chales (40) mkaazi wa Kata ya Katuma wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amekufa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.Tukio okt 12,2017
Ripoti ya Oktoba 9,2017-
MTU mmoja amepoteza maisha kwa madai ya kupigwa risasi na askari wa maliasili na wengine wanne kujeruhiwa katika kitongoji cha Mnyamasi wilayani Tanganyika mkoani Katavi,wakati wa oparesheni ya kuwaondoa wakazi wanaodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi-Tukio Okt 7,2017
MATUKIO YA HIVI KARIBUNI
Ripoti za Oktoba 12,2017
Mtu mmoja anayefahamika kwa jila la Suzani Chales (40) mkaazi wa Kata ya Katuma wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amekufa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.Tukio okt 12,2017
Ripoti ya Oktoba 9,2017-
MTU mmoja amepoteza maisha kwa madai ya kupigwa risasi na askari wa maliasili na wengine wanne kujeruhiwa katika kitongoji cha Mnyamasi wilayani Tanganyika mkoani Katavi,wakati wa oparesheni ya kuwaondoa wakazi wanaodaiwa kuvamia msitu wa hifadhi-Tukio Okt 7,2017
Comments