NDEGE YA MIZIGO IMEANGUKA IVORY COAST
Mabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika ufukwe ambapo waokoaji walionekana wakiwatibu watu walionusurika. |
Mabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika
ufukwe ambapo waokoaji walionekana wakiwatibu watu walionusurika.
Kwa mjibu wa mtandao wa Koac ndege hiyo ilikuwa ikibeba
mizigo ya jeshi la Ufaransa ambapo inasemekana imeanguka wakati wa mvua kubwa
karibu na bandari ya Bouet.
Shahidi mmoja amesema watu wanne walifariki huku miili miwili
ikitolewa kutoka katika ndege hiyo huku mingine miwili ikionekana katika mabaki
ya ndege hiyo.
Vyombo vya habari na tovuti ya Ivoire Matin viliripoti vifo
vya watu watatu huku watu sita wakijeruhiwa ambapo Mtu mmoja amekamatwa na Ndege
hiyo imedaiwa kutengezwa nchini Ukrain.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments