RAIS AMEWAJIBU SHIRIKISHO L VYAMA VY AWAFANYAKAZI TUCTA
Rais
John Pombe Magufuli amesema serikali ya awamu ya tano imewapandisha vyeo na
kurekebisha mishahara ya watumishi 59,967 baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti
feki hewa kukamilika.
Rais
Magufuli amesema hayo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya mbio za Mwenge wa
Uhuru na kumbukumbu za miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere,sherehe ambazo zimefanyika visiwani Zanzibar.
Rais
Magufuli katika hotuba hiyo alitolea mfano uzalendo wa Baba wa Taifa ambaye
aliamua kupunguza mshahara wake na kukataa kuongeza mishahara ya watumishi
wachache huku walio wengi wakipata shida.
“Ninaposema hivyo simaanishi kuwa
mishahara isiongezwe. La hasha. Ninachosema ni kwamba kabla ya kudai nyongeza
ya mishahara ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa Serikali, lakini pia tutambue
kuwa kuna Watanzania wenzetu wengi tu wanaohitaji kuboreshewa huduma.
"Hata hivyo baada ya
kukamilisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na vyeti feki, Serikali
imewapandisha vyeo na kuwarekebishia mishahara watumishi 59,967 ambapo kiasi
cha Shilingi Bilioni 159.33 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka huu na mishahara
mipya itaanza kulipwa kuanzia mwaka huu. Na kwa upande wa Zanzibar kima cha
chini cha mshahara kimeongezwa kutoka Shilingi 150,000/- hadi kufikia Shilingi
300,000/-” Amesema Mhe. Rais Magufuli.
Wiki iliyopita shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA lilikuwa limesema linatarajia kufanya vikao na serikali kujadili tamko la Rais Magufuli kusema kuwa katika kipindi chake chote cha uongozi watumishi wa umma wasitegemee kupandishiwa madaraja na mishahara suala ambalo juzi lilikanushwa na msemaji wa serikali kuwa hakuna kipengele kinachotamka kuwa Rais alisema hataongeza mishahara wala kupandisha madaraja.

Mbali
na hilo Rais Magufuli aliwataka vijana kuendelea kujielimisha katika mambo
mbalimbali na kuwataka kutojihusisha na masuala ya madawa ya kulevya na
kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments