MKUU WA WILAYA MPANDA ATOA SIKU SABA KWA OFISI YA MADINI KUTATUA MGOGORO KATI YA KAMPUNI YA KIJANI INVESTMENT NA WACHIMBAJI WADOGO MPANDA.
Na.Meshack Ngumba-Mpanda
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bwana Pazza Mwamlima ametoa siku saba Kwa ofisi ya
Madini Wilayani Mpanda Kutatua Mgogoro uliopo baina ya Kampuni ya Kijani
Investment na Wachimbaji wadogo wa dhahabu Katika Machimbo ya Dilifu.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima Akizungumza na wananchi waishio katika mgodi wa dhahabu wa Dirifu ambao kipato kikuu wanategemea mgodi huo (PICHA NA Issack Gerald) |
Akizungumza jana Katika Mkutano wa
hadhara na Wakazi wa Kijiji cha dilifu kilichopo Katika Kata Manga Mwamlima amewata
wachimbaji hao kuendelea na shughuli za Uchimbaji wakati Malalamiko yao
yakitafutiwa ufumbuzi.
Uamzi huo umetolewa ikiwa ni siku
Moja baada ya wachimbaji wadogo Katika Machimbo hayo Kuanzisha Maandamano
yasiyokuwa na kikomo kufuatia ofisi ya Madini Mkoani Katavi Kusitisha shughuli za Uchimbaji kuendelea Katika Machimbo hayo kwa madai ya
Kukosa leseni ya Uchimbaji.
Hata hivyo wachimbaji hao wameiomba Serikali
Kushughulikia Migogoro iliyopo baina ya wawekezaji na Wachimbaji wadogo wadogo
inayochangiwa na Kuwepo kwa baadhi ya watumishi wasio waminifu Katika sekta ya
Madini hapa nchini.
Mbali na wachimbaji wa dirifu,pia
kumekuwepo malalamiko ya wachimbaji wapatao 200 katika mgodi wa dhahabu uliopo
mlima wa Kampuni wakilalamika kufukuzwa katika mgodi huo wakati eneo hilo ndilo
tegemeo la takribani miaka 36 iliyopita yaani miaka ya 1980.
Comments