MAHAKAMA YAAMURU NDOA KUVUNJIKA WILAYANI MPANDA,WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SHAMBULIO LA MWILI.
Na.Boniface
Mpagape-Mpanda
MAHAKAMA
ya Mwanzo mjini Mpanda juzi imeamuru mdai Leticia Seleman awe na uhuru wa
kuishi peke yake au kuanzisha mahusiano mengine ya ndoa katika kesi ya madai ya
talaka kutoka kwa aliyekuwa mmewe Makono Brash.
Mahakamani |
Akisoma
hukumu hiyo, hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela amesema mahakama imeona
mdai Bi. Leticia Seleman hastahili kupewa talaka baada ya kushindwa
kuithibitishia mahakama kama kuna ndoa inaendelea kati yao.
Madai
hayo ya talaka yanatokana na Mdai Bi. Leticia Seleman kutaja sababu ambazo ni
pamoja na kutelekezwa kwa muda mrefu, kutishiwa kuuawa na kwamba mdaiwa Bw.
Makono Brash ameuza mazao na ng’ombe mali ya mdai.
Hukumu
hiyo imetolewa katika mahakama hiyo bila uwepo wa mdaiwa licha ya kutumiwa wito
kufika mahakamani hapo mara mbili na hakufika. Hakimu Mbembela amesema mdaiwa
hakuwahi kufunga ndoa na walitengana tangu mwaka 2008 na katika maisha yao ya
ndoa walipata watoto sita wanaoishi na mama yao.
Amesema
ili mdai awe na uhuru huo, lazima kwanza uhusiano wa ndoa uvunjwe na mahakama
kwa mujibu wa sheria. Mahakama hiyo imeona sababu zilizotolewa na mdai
zinaangukia kwenye makosa ya ukatili wa kimwili na kisaikolojia, hivyo uhusiano
wa ndoa umevunjika kiasi cha kutorekebishika.
Katika
shauri jingine lilifikishwa katika mahakama hiyo jana, Watu watatu wa familia
moja wakazi wa kamakuka Mnyagala wilayani Mpanda wameshtakiwa kwa kosa la
shambulio la kudhuru mwili na kusababisha upotevu wa mali.
Imeelezwa
mahakamani hapo na WP 9737 PC Elly Neema kutoka jeshi la polisi Mpanda mbele ya
hakimu wa mahakama hiyo Bw. Mkumbi Ramadhani Mumbi kuwa , washatakiwa hao
ni Nogi Kahindi, Shilinde Nogi na Joseph
Nogi na walitenda kosa hilo tarehe 03 mwezi Oktoba mwaka 2015 usiku majira ya
saa nane, walimvamia mlalamikaji Jitobelo Ngalula ambaye ni mfugaji, na kuanza
kumshambulia kwa fimbo huku wakihoji kwa nini amekataa kuhama katika eneo
analoishi na wakati huo huo akimiliki eneo hilo kwa miaka sita sasa.
Akitoa
ushahidi mbele ya mahakama, Mlalamikaji Bw. Jitobelo Ngalula aliwajibu kuwa
eneo hilo wamekabidhiwa na serikali na waliendelea kumshambulia na
kumsababishia majeraha kichwani, mkononi na mguuni na kusababisha upiotevu wa
fedha shilingi laki moja na elfu hamsini, na simu aina ya Tecno yenye thamani
ya shilingi elfu themanini.
Amesema
baada ya kushambuliwa ilimlazimu akimbilie porini baada ya jirani yake kufika
eneo la tukio na kuhoji sababu za kumshambulia kwa fimbo.
Washtakiwa
wote wamekana shtaka dhidi yao na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe nane mwezi
Machi mwaka huu, na mahakama hiyo imeruhusu dhamana ya ahadi ya shilingi laki
tano kwa kila mmoja na endapo hawatatimiza masharti ya dhamana warudishwe
rumande hadi tarehe iliyopangwa.
Comments