BENKI YA DUNIA KUFADHIRI UJENZI WA KILOMITA 7.7 ZA BARABARA MANISPAA YA MPANDA 2016/2017
Na.Issack Gerald-Mpanda
Zaidi
ya kilometa 7.7 za barabara katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,zimetengwa
kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami
kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Benki ya dunia |
Taarifa
ya ujenzi wa barabara hizo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Manispaa ya Mpanda Bw.Hamis Mkele, wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamaba na Mpanda Radio kwa njia ya simu.
Mkele
amesema kuwa ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu unadhaminiwa
na benki ya dunia.
Aidha
amesema kuwa amesema ujenzi wa barabara
hizo hautafanyika kwa pamoja kutokana na fungu la fedha watakalopatiwa kutoka
benki hiyo kutokuwa na uhakika kama litatosheleza mahitaji.
Baadhi
ya Barabara hizo zinazotarajiwa kujengea kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara
ya Afya Dispensal hadi Istiqama,Hospital ya Wilaya hadi Istiqama,kutoka Shule
ya Sekondari St.Mary’s hadi madukani na barabara zinazozunguka eneo la mitaa ya
Kashaulili.
Mara kwa mara wakazi wa Manispaa ya Mpanda wamekuwa
wakilalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayowapa taabu ya kupita
kuelekea wanakohitaji kupatiwa huduma ikiwa ni pamoja na Hospitalini kutokana
na barabara zilizo nyingi kutopitika hususani msimu wa masika.
Benki ya Dunia ni taasisi ya kimataifa yenye
shabaha ya kusaidia maendeleo ya nchi za dunia. Si benki ya kawaida.
Inashirikiana na Umoja wa Mataifa na hasa Shirika la Fedha la Kimataifa lakini si
chini ya UM moja kwa moja. Ni mali ya nchi wanachama 185 zinazopigia kura
katika mikutano yake kulingana na thamani ya hisa zao katika rasilmali ya
benki.
Comments