MAFUNZO YA SIKU 3 KUHUSU UTUNZAJI WA FEDHA NA MALI ZA UMMA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YAANZA KATAVI.
Na.Issack Gerald-Katavi
MAHAKAMA
ya Tanzania imeanza mafunzo ya siku 3 kuanzia leo hadi February 27 juu ya utunzaji
wa fedha na mali ya umma kwa watumishi wa mahakama ya Tanzania mkoani Katavi
katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda.
Mtendaji
wa mahakama ya Tanzania mkoani Katavi Bw. Ipyana Isaac Kakuyu, amesema mafunzo
hayo yamejumuisha watumishi wa kada za uhasibu, ugavi, utumishi pamoja na
Teknolojia ya habari na mawasiliano -Tehama.
Amesema
mafunzo haya yanalenga kuwajengea zaidi uwezo wa kuelewa masuala muhimu yanayohusu
utunzaji wa fedha na mali ya umma pamoja na kanuni na taratibuza manunuzi kama
ilivyoainishwa katika sheria ya fedha ya namba 6 ya mwaka 2001 iliyoboreshwa
mwaka 2004 na sheria ya manununzi ya umma na.7 ya mwaka 2001 paoj ana kanuni na
taratibu za manunuzi za mwaka 2013 ili kuongeza utdhibiti na uwajibikaji katika
kusimamia.
Ametaja
changamoto zinazowakabili kuwa ni uhaba wa watumishi wa kusimamia rasimali za
umma, pamoja na kanuni na taratibu za manunuzi kukosekana katika mahakama ya
mkoa wa Katavi .
Washiriki
katika mafunzo hayo ni pamoja na Mkuu wa Hazina ndogo Mkoani Katavi,Mkaguzi
Mkazi kutoka Ofisi ya taifa Mkaguzi na mdhibiti Mkuu Mkoani Katavi Bw.Philbert
Kanyogozi,Mhakiki mali mwakili Mkoani Katavi Bw.Julius Mwanganikani,Hakimu
mkazi mfawidhi Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa,Mkaguzi wa ndani kutoka ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na wajumbe mbalimbali.
Comments