MTOTO MWENYE MIAKA 03 AUWAWA KIFO CHA UTATA KATAVI,WAZAZI WAKAA NA MAITI NDANI YA NYUMBA KWA SIKU 4,MAJIRANI WARIPOTI TUKIO POLISI BAADA YA KUKERWA NA HARUFU MBAYA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Katavi
WATU wawili ambao ni wazazi wa mtoto
aliyefahamika kwa jina la Justina Laurent (3) wanashikiliwa na jeshi la polisi
Mkoani Katavi kwa kusababisha kifo cha mtoto huyo ambaye aligundulika akiwa
amefariki dunia ndani ya chumba cha wazazi wake huku akiwa na majeraha sehemu
mbalimbali za mwili wake.
Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi
Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Februari
24 katika mtaa wa Mji wa Zamani Kata ya Kashaulili Wilayani Mpanda.
ACP Mohamed amewataja wazazi hao kuwa
ni Mariam Elias (20) na Juma Suleiman (24) wote wakazi wa mtaa wa Mji wa
Zamani.
Aidha
Kamanda Mohamed amesema kuwa Mwili wa marehemu umeonekana ukiwa na majeraha sehemu
za kichwani, miguuni, mbavuni, tumboni na mikononi majeraha ambayo yanatiliwa
shaka huenda yakawa ya kuunguzwa na moto ama ugonjwa wa ngozi.
Katika
mahojiano ya awali na wazazi wa mtoto huyo walikiri kwamba marehemu alianza
kuugua ugonjwa wa ngozi tangu tarehe 18.02.2016 lakini hawakuwahi kumpeleka
hospitali
Hata
hivyo Mpaka sasa chanzo cha majeraha hayo yaliyosababisha kifo chake bado
kujulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa
wito kwa wananchi kuwa na kawaida ya kutoa taarifa yoyote inayotiliwa shaka
kwenye vyombo vya dola ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa haraka na kwa wakati
lakini pia ameiasa jamii kuacha kushiriki kufanya vitendo vya kishirikina.
Kwa upande wa majirani wa familia
hiyo wamesema kuwa mwili wa marehemu umekuwa ndani ya nyumba kwa siku ya nne
hadi leo tangu kuuwawa kwa mtoto huyo na harufu mbaya iliyokuwa ikitoka ndani
ya nyumba ya watuhumiwa ndiyo imepelekea kupeleka taarifa polisi na hatimaye
upekuzi kufanyika na kugundua mwili huo.
Comments