WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA,DC ATOA KAULI
Na.Issack Gerald
Mkuu wa
wilaya ya mpanda Liliani Charles Matinga ameamuru masoko yote kufunguliwa baada ya wafanyabiashara kufanya mgomo kutokana na ongezeko la tozo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kodi.
Amri
hiyo ameitoa leo asubuhi wakati akiwa soko kuu
ambapo wafanyabiashara waliogoma
kufungua biashara zao huku akisema kwa anayeshindwa arudishe chumba cha biashara.
Amesema
wamekaa na wafanyabiashara kwa ajili ya kupanga ongezeko hilo ambapo hapo awali
halimashauri ilipanga laki moja na baada ya hapo ikapungua hadi elfu sitini.
Awali
wafanya biashara hao wamesema walishindwa kumudu kodi iliyokuwepo ya shilingi
15000 ambapo wamesema serikali kuwatoza shilingi 60000 ni kuendelea
kuwakandamiza.
Masoko
amabyo wafanyabiashara wamefunga biashara zao ni Soko kuu la Wilaya ya Mpanda na
Soko la Buzogwe lenye zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 500 hii ikiwa ni kwa
mjibu wa baadhi ya wafanyabiashara.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments