SERIKALI MKOANI MTWARA KUTOWACHUKULIA WANAFUNZI WAJAWAZITO

Serikali imesema haitawafungulia mashtaka wasichana watano wa shule waliopata ujauzito ambao walikamatwa mwishoni mwa juma lililopita baada ya mkuu wa wilaya kuagiza kukamatwa kwao.
Hatua hiyo iliibua mjadala mkali huku wanaharakati wa kijamii wakipinga hatua hiyo ya serikali wakisema kuwa agizo hilo inakandamiza haki za watoto hao.
Wanaharakati wanaohusika na utetezi wa haki za watoto na wamesema uamuzi wa kuwakamata wazazi hauwezi kuwa njia pekee ya kutokomeza mimba za utotoni bali serikali inapaswa pia kuangazia visababishi vingine vinavyochangia ongezeko la mimba za utotoni.
Afisa katika shirika la kupigania haki za wanawake Tanzania TAMWA Edison Sosten amesema Kuna vikwazo vingi ambavyo mabinti wanakutana navyo katika mazingira ya nyumbani pia wakati akitoka shuleni.
Katika suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byankwa maamuzi hayo yanalenga sio kuwaadhibu wazazi bali kujenga ushirikiano nao kwa sababu wengi wamekuwa wakificha majina ya watu waliowapatia mimba watoto kwa sababu ya kufahamiana nao.
Kwa mujibu wa shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch,nchini Tanzania zaidi ya watoto 15,000 hukatisha masomo yao kila mwaka kutokana na mimba za utotoni.
Aidha kwa mujibu ya utafiti wa afya uliotolewa na wizara ya afya mwaka 2015 hadi 2016,asilimia 27 ya watoto wa kike wamepata watoto wakiwa kati ya miaka 15 na 19.
Mwezi Agosti Mwaka uliopita,Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alitoa marufuku kwa wasichana wanaopata ujauzito kuendelea na masomo katika shule za serikali.
Chanzo:bbc
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA