MATOKEO YA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI YATANGAZWA
Baraza
la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa
darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana huku
idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.
Akitangaza
matokeo hayo leo,Katibu Mtendaji wa Necta, Dk.Charles Msonde amesema
jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne
wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
Amesema
wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati
wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni
ufaulu usioridhisha.
Kuhusu
matokea ya upimaji wa kidato cha pili,Dk Msonde amesema jumla ya
wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa
kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na
kidato cha tatu.
Dk
Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68
wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments