RAIS MAGUFULI AIPA SIKU 5 WIZARA YA KILIMO,WAZIRI MTEGONI
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa katika mikoa yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo Mkoa wa Rukwa ifikapo Ijumaa Januari 12, 2018.
Magufuli
ameyasema hayo leo wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu
Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amemuelekeza
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kufuatilia jambo hilo na amebainisha kuwa endapo
mbolea haitafikishwa katika maeneo hayo ifikapo Ijumaa wahusika waachie ngazi.
Rais
Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo
na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote atakayeshindwa
kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments