KIDATO CHA KWANZA WARIPOTI KWA KASI KATIKA SHULE MBALIMBALI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha
kwanza ambao wameripoti katika shule mbalimbali za sekondari Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi,wamesema wamejiandaa kusoma kwa bidi ili kuwa na ufaulu mzuri kitaaluma.
Miongoni mwa Wanafunzi katika Shule ya
Sekondari Mwangaza wamesema wamejiwekea mikakati yao kuhakikisha wanafaulu kwa
kiwango kinachotakiwa kitaaluma ambapo wanafunzi hao wanatoka katika shule mbalimbali
za msingi zikiwemo Kawanzige,Kakese,Mwangaza,uhuru, Kashato,Kashaulili na Katavi.
Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari
Mwangaza iliyopo Manispaa ya Mpanda Simon Lubange amesema,mpaka sasa wanafunzi karibu
ya 200 kati ya 260 wanaotakiwa kuripoti katika shule hiyo wameripoti ili kuanza
masomo.
Nao baadhi ya wazazi ambao wamewapeleka
shule watoto wao wamesema ni wakati wa kila mzazi kutambua umuhimu wa elimu kwa
kila mtoto kwa maisha ya baadaye.
Hata hivyo kwa mjibu wa takwimu iliyotolewa
mwaka uliopita na Afisa elimu Mkoani Katavi Ernesti Hinju inaonesha zaidi ya wanafunzi
9000 wanalizimika kutojiunga mapema na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka
2018 kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments