TEHERAN
Afisa wa ngazi ya juu
katika sekta ya elimu nchini Iran ametaka lugha ya Kiingereza isiendelee
kufundishwa katika shule za msingi nchini humo.
Katika mahojiano na
kituo cha televisheni ya taifa ya Iran jana Jumapili, afisa huyo, Mehdi
Navid-Adham ambaye ni kiongozi wa Baraza la Elimu ya Juu amesema Kiingereza ni
mkondo wa uvamizi wa kitamaduni wa nchi za Magharibi.
Mwaka 2016 Kiongozi
Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitoa mapendekezo kama hayo, baada ya
kuarifiwa kuwa baadhi ya shule za chekechea zilikuwa zikiwafundisha watoto kwa
lugha ya Kiingereza.
Tangazo hilo limekuja
wiki moja baada ya maandamano dhidi ya serikali kulalamikia hali ngumu ya
uchumi, maandamano ambayo Khamenei alisema yaliratibiwa kutoka nje ya nchi.
Comments