WALIMU WAKUU MKOANI TABORA WALALAMIKIA UFINYU BAJETI YA RUZUKU YA ELIMU BURE-Oktoba 5,2017
Na.Issack Gerald
WAKUU
wa shule wamelalamikia kutotosheleza kwa kiwango cha fedha ambacho kimekua
kikitolewa na serikali kuu kwamba hakikidhi mahitaji na wameiomba serikali
kuongeza kiwango cha fedha ambazo zimekua zikitolewa kama ruzuku kwa
ajili ya kusaidia wanafunzi mashuleni.
Hayo
yamebainishwa katika mkutano ambao umewakutanisha wadau mbalimbali wa elimu
katika ukumbi wa chuo cha veta mjini Tabora kupokea mrejesho wa ufuatiliaji wa
matumizi ya fedha za ruzuku kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Mkutano
huo umeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali ya Haki elimu kwa kushirikiana
na mtandao wa marafiki wa Elimu Mkoani Tabora.
Miongoni
mwa mambo ambayo yamejadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na suala la sera ya elimu bure huku baadhi ya walimu
wakitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuongezea fedha za ruzuku kwa ajili ya
kuendesha maendeleo ya shule kwa kuwa fedha ambayo imekuwa ikitolewa na
serikali kuu inakuwa haijitoshelezi.
Kwa
upande wake Imani Mwakalinga ambaye ni mwenyekiti wa mtandao wa elimu Mkoani
Tabora amesema kuwa bado kuna changamoto ya matumizi ya fedha hizo ambapo
wananchi kwa kiasi kikubwa hakuna uwazi wa taarifa za mapato na matumizi kwa
kuwa hata ushirikishwaji wa wananchi umekuwa mdogo kwani hakuna fedha
zinazochangwa na wananchi kwa kiwango kikubwa.
Naye
mbunge wa jimbo la Tabora Mjini Emmanuel Mwakasaka amesema bado wananchi wana
nafasi ya kushirikishwa katika michango ambayo siyo mikubwa kwa ajili ya
maendeleo ya shule.
Aidha
zaidi ya Shilingi Milioni 236 zimekuwa zikitolewa na serikali kwa ajili ya
uendeshaji wa sera ya elimu bila malipo kwa shule za msingi 76 na shule za
sekondari zipatazo 23 zilizopo Mkoani Tabora.
huku
wananchi.
Mwandishi:Amisa Mussa,Mhariri-Issack
Gerald
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments