JESHI LA POLISI MKOANI RUKWA WATAJA MAJINA YA WALIOKUFA KATIKA AJALI-Oktoba 5,2017
Na.Issack Gerald-Sumbawanga
JESHI
la polisi mkoani Rukwa limetoa majina ya watu 15 waliofariki katika ajali ya
Fuso lenye namba za usajili T425 BFF ili ndugu zao wakachukue miili ya marehemu
kwaajili ya kwenda kufanya maziko.
Kamanda
wa polisi mkoani humo Georege Kyando alisema kuwa miili ya watu waliokufa
katikaajali hiyo ni wanawake 10 nawanaume watano huku baadhi ya ipo
katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Nkasi.
Aliwataja
marehemu hao kuwa ni Domona Tenganamba(41),Emaanuel Rashif(84),Restuta
Sunga(35) Salula Revena(38)FeresiaTenganamba(12)
Prisca
Madeni(45).
Aliwataja
wengine kuwa ni mwalimu washuleya msingi Kalambanzite, Richard
Chikwangara(24)Yusta Somambuto(36),Giles Ramadhani(24),
Odetha
Madirisha(46)Megi Nalunguli(52)
Kamanda
Kyando Aliwataja wengine kuwa ni Abuu Amani Mandevu(37)Nyandindi Batrahamu(35)
Magdalena Mbalamwezi(50) pamoja na mtoto mwenye umri wa wiki mbili ambaye bado
hajapewa Jina.
Pia
aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Dismas Clement(26),Sema Savery(25)Ally
Haruna(33),Yusta Mfundimwa(50)Tenesfory Oscar(36) Amos Kitambale(25) Neema
Mwanandenje(21)Joseph Sungula(28) namwanamke mmoja ambaye Yupo chumba cha
wagonjwa mahututi I. C. U na hajafahamika jina lake mpaka sasa.
Alisema
kuwa marehemu na majeruhi wa ajari hiyo ni watu kutoka katika mikoa mbalimbali
hapa nchini ni vizuri wananchi wakafuatilia ili kujua kama kuna ndugu yao
wafanye mawasiliano kwani serikali iliahidi kusafirisha maiti mpaka
watakapofanya maziko.
Alisema
kuwa dereva wa gari hilo bado anasakwa na atakapopatikana afikishwe mbele ya
sheria kwa uzembe nakusababisha ajali iliyo sababisha vifo hivyo.
Naye
mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mtanda alimshukuru rais John Magufuli kwa
kuungana na wafiwa wote katika katika kipindi hiki cha majonzi kwa kuondokewa
na ndugu zao kwa ajali mbaya ya gari.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments