KAMATA KAMATA WASIOKUWA NA VYOO MKOANI MBEYA-Oktoba 5,2017
Na.Issack Gerald
WANANCHI wa Halmashauri ya Busokelo
Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wanakabiliwa na ukosefu wa vyoo bora.
Katika kukabiliana na hali hiyo,Halmashauri imeanza kuchukua hatua za kuwafikisha Mahakamani wananchi wasiokuwa na vyoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya
Wilaya ya Busokero Eston Ngilangwa amesema Kampeni ya usafi itakuwa endelevu
huku akisema kuwa amepata upinzani kutoka kwa wananchi kuhusu suala la usafi
huku akisema hata lifumbia macho.
Aidha amesikitishwa na baadhi ya wanasiasa
wanaopinga hatua anazochukua dhidi ya wananchi wasiokuwa na vyoo wakisema kuwa
watakosa kura kipindi cha uchaguzi.
Hata hivyo amesema hatasita kuchukua
hatua kwa mtu yeyote atakayekwamisha suala la vyoo na atachukua hatua bila
kujali cheo au wadhifa alionao.
Halmashauri ya Busokero inashika
nafasi ya 182 kwa kusafi kati ya Halmashauri 185 zilizopo nchini ambapo
Halmashauri hiyo ina historia ya kukumbwa na ugonjwa kipindupindu mwaka 2016.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments