CWT KATAVI WAICHARUKIA SERIKALI SUALA LA STAHIKI ZAO-Oktoba 5,2017
Na.Issack Geral-Katavi
CHAMA cha walimu Tanzania CWT mkoani
Katavi,kimeitaka serikali kulipa madeni pamoja na malimbikizo mbalimbali ya
walimu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha walimu Tanzania CWT Mkoa wa
Katavi Hamisi Ismaili ikiwa leo ni siku ya walimu Duniani.
Amesema serikali imekwishafanya
uhakiki wa Madeni hayo ya walimu hivyo kama imeridhishwa ni vema kulipa kwani
walimu wameanza kukata tamaa.
Wakati
huo huo baadhi ya walimu kutoka shule mbalimbali za Manispaa ya Mpanda,wamesema
kukosekana kwa mazingira rafiki ya kazi ni kikwazo katika kuwaandaa wanafunzi
watakaoleta tija kwa taifa.
Madai
haya yanajiri ikiwa ni siku chache tu tangu Rais wa Tanzania DK John Pombe
Magufuli kusema hana mpango wa kuongeza mishahara.
Tamko
hilo la Rais limwaacha wengi wa watumishi wa umma wakishangaa kauli ya rais
inayoleta mkanganyiko tofauti na kauli aliyokuwa ameitoa awali mei mosi siku ya
wafanyakazi duniani kuwa kuanzia mwezi julai katika mwaka wa fedha
2017/2018,serikali italipa mishara kwa wakati,itaongeza mishahara kwa watumishi
wa umma,kupandisha madaraja na kulipa malimbikizo ya madeni yote inayodaiwa
serikali.
Hata
hivyo shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limesema limeshtushwa
na tamko la rais John Magufuli na ambapo wamesema wanatarajia kukutana ili
kujadili tamko hilo ikiwa ni pamoja na kuketi kiti kimoja na serikali kwa ajili
ya maslahi ya watumishi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania limited Group
Comments