FUSO YAUA 15 YAJERUHI 19 MKOANI RUKWA-Oktoba 5,2017
Na.Issack Gerald-Sumbawanga
Watu 15 wamefariki dunia na wengine
19 kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari la mizigo aina ya Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Geoge
Kyando amethibitisha tukio hilo na kusema Lori hilo aina ya Fuso likiwa
limebeba shehena ya viroba vya mahindi na watu 28 ndani yake limepinduka baada
ya dereva kukata kona akiwa kwenye mwendokasi na kupelekea vifo hivyo.
Amesema gari hilo lilikuwa likitoka
Sumbawanga kuelekea Wampembe katika mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani Nkasi
mkoani Rukwa usiku wa kuamkia jana.
Aidha Kamanda amesema Mbali na
barabara kuwa ya milima na mteremko mkali kutajwa kuwa mojawapo ya chanzo cha
ajali pia inasemekana dereva aliugua ghafla gari likiwa katika mwendo.
Hata hivyo dereva aliyekuwa
anaendesha baada ya Yule wa awali kuugua,ametoweka kwa kukimbilia
kusikojulikana baada ya ajali ambapo mmliki wa gari anasakwa na polisi ili
sheria ichukue mkondo wake kufuatia gari hilo kubeba abiria kinyume na
utaratibu wa magari yanayotakiwa.
Maiti 14 zimetambuliwa isipokuwa mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina Abubakari Amani(Madevu) hajatambulika ambapo maiti
zote zimehifadhiwa katika hospitali ya mkoa waRukwa.
Mwezi uliopita watu watatu walifariki
dunia na wengine watatu walijehiwa kufuatia ajali ya kupinduka kwa lori na mtu
kugongwa huku ajali nyingine ya boti iliyosababisha vifo vya watu ikitokea ziwa
Tanganyika.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments