RC MUHUGA AKABIDHA MAJIKO BANIFU KWA SHULE ZA SEKONDARI RUNGWA NA MPANDA GIRLS-Oktoba 5,2017

Na.Issack Geral-Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,amekabidhi majiko banifu manne yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne kwa shule za sekondari Rungwa na Mpanda Girls.

Akikabidhi majiko hayo ambayo yametolewa na mradi wa Usimamizi endelevu wa misitu ya miombo Tanzania,Muhuga amesema majiko hayo yanalenga kupunguza uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa usimamizi endelevu wa misitu ya miombo taifa NPC Bw.Yobu Kiungo amesema, katika Mkoa wa Katavi mradi huo unatekelezwa Wilayani Mlele ambapo shule hizo zimepata majiko kutokana na kuwa katika makao makuu ya mkoa.
Awali akisoma taarifa ya mkoa,kaimu katibu tawala Msaidizi Mkoani Katavi Mhandisi Awariywa Moses Nnko amesema kwa mwaka 2017 mradi huo umewezesha majiko 983 yenye thamani ya shilingi milioni sitini yamewezeshwa katika taasisi za serikali na kaya binafsi.
Aidha Nnko amesema kuwa mwaka 2015/2016 mradi uliwezesha mashine mbili za umeme na mashine tanzu kwa ajili ya kuzalisha mkaa mbadala huku mwaka 2016/2017 mradi uliwezesha mtambo wa gesi asilia katika shule ya Sekonadri Inyonga kwa ajili ya kupika na matumizi ya maabara.
Wakati huo huo kwa Mwaka 2016/2017 mradi umewezesha majiko banifu 595 ya kiwemo ya kaya 7,Shule ya Mingi mtakuja jiko 1 na Shule ya Sekondari Inyonga 2.
Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Rungwa Emmanuel Cassian Mwamwezi na Nyabisye Sabasi mkuu wa Sekondari ya wasichana Mpanda Girls wamesema majiko hayo yamesaidia kurahisisha upishi wa vyakula vya wanafunzi na kutunza mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni.
 Mradio huo ulio chini ya Mpango wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa UNDP pia unatekelezwa mkoani Tabora.
Dada mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mpanda Girls Delila Ebanda akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo,asema majiko hayo watayatunza vizuri ili yatumike kwa wanafunzi watakaokuwepo katika shule hiyo hata baada ya wanafunzi waliopo kuhitimu.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Mwalimu Enelia Lutungulu,Afisa elimu wa Mkoani Katavi Ernest Hinju na wataalamu wengi wa elimu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda walikuwepo huku Manispaa ikiahidi kutunza majiko hayo.
Shule ya sekondari ya Rungwa yenye jumla ya wanafunzi 838 kati yao wasichana wakiwa ni 386 na wavulana 432 ina walimu 40 huku kwa upande wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mpanda Girls iliyoanzishwa Februari 25 mwaka 1986 kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 981 na walimu 40 kati yao walimu wa kike wako 9 na wa kiume 31.
Shule ya sekondari Mpanda Girls yenye mchepuo wa Tahasusi za PCB , PCM, CBG, EKA,HGE, EGM, HKL, HGK, NA HKL inafundisha masomo ya sayansi,uchumi na sanaa ambapo mwaka 2011 serikali iliipandisha hadhi ya kuchukua wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 ambapo kuanzia mwaka 2005 ilikuwa ikichukua wanafunzi wa kidato cha tano pekee na kufundisha tahasusi ya HGK.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania limited Group

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA