DC MLELE AFUNGUA MAFUNZO YA UANDAAJI BAJETI KISASA-Oktoba,5,2017
Na.Issack
Gerald-Mpanda Katavi
MKUU wa Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi
Recho Kasanda,leo amefungua mafunzo ya siku tano ya uandaaji bora wa bajeti
unaojulikana kama PLANEP kwa wakuu wa idara katika Halmashauri hiyo pamoja na
wafanyakazi waandamizi ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mlele.
Katika mafunzo hayo ambayo
yamefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Inyonga,Kasanda amesema mfumo
huo utaongeza uwazi,uwajibikaji pamoja na kupunguza gharama za serikali katika
halamshauri hiyo.
Mfumo huo wa bajeti kwa njia ya
kielektroniki unatarajiwa kutumika kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019.
Mafunzo hayo yaliyoanza Jumatatu ya
wiki hii yatahitimishwa kesho.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments