ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA
Jaji
mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amesema katika kuadhimisha siku ya sheria
Nchini ,mahakama imekusudia kuandaa maonesho maalumu kwa ajili ya kutoa elimu
ya sheria kwa wananchi ili kupunguza uvunjifu wa sheria.
Akizungumza
na waandishi wa Habari kuhusiana na shamrashamra za siku ya Sheria Jaji makungu
amesema maonesho hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu pia yatawapa fursa
wafanya bishara kuuza biashara zao.
Amesema
mbali na Maonesho hayo pia Kutakuwa na Ufunguzi wa Mahakama ya Wilaya
ya mwanakwerekwe baada ya kumalizika kwa ukarabati wa Mahakama hiyo ambayo
itafunguliwa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Muhammed Shein.
Aidha
amesema katika shamrashamra hiyo kutakuwa na matembezi ya siku ya sheria yatayoongozwa
na Spika wa baraza la wawakilishi kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujua
umuhimu wa kufuata sheria.
Akizungumzia
mafanikio waliyapata katika uendeshaji wa kesi kwa wananchi hususan kesi za
Udhalilishaji amesema mpaka sasa usimamizi wa kesi unakwenda vizuri jambo
ambalo linapelekea wananchi kunufaika na haki zako za msingi licha ya kuwepo
kwa mapungufu katika masuala ya ushahidi.
Amesema
wananchi wamekuwa na mwamko wa kuripoti kesi hizo lakini zinashindwa kuendelea
kutokana na wananchi kushindwa kuleta ushahidi kwa wakati na kusababisha ugumu
katika utoaji wa maamuzi.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na uingizwaji na Usambazaji wa dawa za
kulevya jaji Makungu amesema bado kuna ugumu katika uendeshaji wa kesi za
madawa ya kulevya kutokana kesi nyingi hazijapatiwa hukumu kwa kukosekana kwa
ushadi.
Siku
ya sheria nchini huadhimishwa kila ifikapo Feb12 ya kila mwaka ambapo kwa
Zanzibar itaadhimishwa katika Ukumbi wa Barza la wawakilishi la Zamani Mjini
unguja na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’kuimarisha utawala wa sheria
kwa kukuza Uchumi wa Nchi’’.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments