ANC CHAZIDISHA SHINIKIZO DHIDI YA ZUMA MGUU SAWA KATIKA MKUTANO WA KESHO
Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC
kimeitisha mkutano wa viongozi wake wa juu utakaofanyika kesho huku kukiwa na
taarifa kwamba mkutano huo ni kwa ajili ya kujadili shinikizo la kumtaka rais
Jacob Zuma kuachia madaraka.
Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho
walilazimika kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya
rais Zuma.
Kwa upande wake rais Zuma ameshikilia msimamo wake
kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.
Mwezi Disemba mwaka jana Ramaphosa alimrithi rais Zuma katika
nafasi ya juu ya kukiongoza chama hicho kikongwe barani Afrika.
Nafasi ya urais ya Zuma imekuwa ikiandamwa na kashfa za
rushwa, ambapo katika miaka ya hivi karibuni alihusishwa na familia yenye asili
ya India ijulikanayo kama Gupta ambapo inadaiwa alitumia madaraka yake vibaya
ili kujinufaisha yeye na washirika wake hao.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments