JUMUIYA YA ULAYA (EU) WAMTEMBELEA TUNDU LISSU KUMJULIA HALI
Maofisa
watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) jana Februari wamemtembelea Mbunge wa
Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini
Ubelgiji.
Lissu
alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30,Septemba 7 mwaka jana na kupelekwa
Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi
alipolazwa hadi Januari 6,mwaka huu alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya
Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Februari 5,2018 Lissu
amewataja maofisa hao kuwa ni Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki
katika Wizara ya Nje ya EU,Patrick Simonnet.
Wengine
ni Mkuu wa Dawati la Tanzania katika EU,Marta Szilagyi,Vania Bonalbert ambaye
ni ofisa wa ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na
haki za binadamu na Hortensia May Lyatuu.
Amesema
ujumbe wa maofisa hao mbali ya kumjulia hali walifanya mazungumzo ya masuala
mbali mbali yanayohusu Tanzania.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments