NDEGE MPYA ZA SERIKALI SASA KULETWA MWEZI JULAI 2018.




Ndege mbili moja aina ya Bombardier na nyingine kubwa Boeing 787 yenye uwezo wa kubeba abiria 262 zilizonunuliwa na serikali zinatarajiwa kuwasili nchini Julai mwaka huu.

Serikali imenunua ndege hizo ikiwa ni mkakati wa kuimarisha Shirika la Ndege (ATCL) ili limudu ushindani kwenye biashara ya kusafirisha abiria na kujiendesha kwa faida.
Akiwasilisha taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha Januari 2017 hadi jana,Mwenyekiti wa kamati hiyo,Prof.Norman Sigalla, alisema wamejulishwa kuwa pamoja na ndege mbili mpya aina ya Dash 8 Q400,Julai serikali inategemea kupokea ndege zingine mbili ambapo moja ni Dash 8 Q400 na nyingine aina ya Boeing 787.
Alisema kwa sasa ATCL ina ndege tatu zinazofanya safari ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine Prof.Sigalla pia alisema Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inashauriwa kuhakikisha viwanja vya ndege visivyokuwa na hati vinapimwa kisha kupatiwa hati miliki.
Alisema viwanja hivyo pia vinapaswa kuwekewa uzio kuepusha uvamizi wa maeneo jambo ambalo huleta migogoro na wananchi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA