WAKAZI WILAYANI MPANDA SERIKALI IWAJIBIKE KUTENGA MAENEO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Magamba Manispa ya Mpanda mkoani Katavi wameitaka serikali
kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima ili kuepusha migogoro ya ardhi
inayojitokeza mara kwa mara
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wakulima na wafugaji wanapoendesha shughuli
zao katika eneo moja huchangia mifarakano isiyo ya lazima na kushauri wafugaji
kutengewa eneo tofauti na wakulima ili kuondoa mwingiliano
Kwa
upande wake Bi.Anna Thomas ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magamba amekiri
kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulima na wafugaji na kuongeza
kuwa inachangangiwa na wafugaji kuwa na mifugo mengi kwenye eneo dogo
Philemone
Tesha Afisa kilimo wa kata ya magamba amesema serikali ina mpango wa kutenga
maeneo ya kuchungia yatakayokuwa tofauti na mashamba japo hakubainisha wazi
mpango huo ni lini utaanza kutekelezwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments