DK.SHEIN ATUNUKU NISHANI ZILIZOTUKUKA 43
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali
Mohammed Shein ametunuku nishani zilizotukuka 43 kwa viongozi na watumishi wa
umma ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Dkt.Shein
ametoa nishani hizo kwa mutu ambae aliasisi,alishiriki na kutukuza pamoja na
kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea mwaka 1964.
Pamoja
na hayo Dk. Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na
utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji
miradi mikubwa ya maendeleo visiwani .
Katika
maadhimisho hayo mbali ya nishani hizo serikali ya Zanzibar huzindua miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ishara ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya
kiuchumi ya taifa hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments